TANGAZO LA ZABUNI

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram

Seventh-day
Adventist Church

TANGAZO LA ZABUNI
ZABUNI NA. UPH/WRH/C/01

Bodi ya Ufunuo Publishing House kwa niaba ya The Registered Trustees of the Seventh-day
Adventist Church of Tanzania, inakusudia kujenga kiwanda kipya cha uchapishaji eneo la
Kitungwa Manispaa ya Morogoro.

Njia ya ununuzi itakayotumika wakati wa ujenzi ni “Force Account” kwa kuzingatia maelekezo ya matumizi ya njia kwa mujibu wa maamuzi ya yaliyofanyika katika vikao vyake.

Bodi ya Ufunuo Publishing House inawatangazia Wananchi, Makampuni a Taasisi mbalimbali
kuomba kazi za ufundi katika ujenzi wa kiwanda tajwa hapo juu.

Masharti muhimu ya zabuni

  1. Iwe ni kampuni ya kitanzania
  2. Waombaji wawe wamesajiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
  3. Awe amesajiliwa na bodi ya wakandarasiTanzania( CRB)
  4. Muombaji aweze kutoa risiti ya EFD na risiti ya kukiri andmapokezi
  5. Bodi ya Ufunuo hailazimiki kukubali kima cha juu wala cha chini cha bei ya mzabuni.
  6. Waombaji wawe na leseni na uzoefu wa miaka mitatu (3) au 1. Zaidi.
  7. Mwombaji aambatishe udhibitisho wa uzoefu aliyonayo katika ujenzi wa viwanda na
    godauni( ware house).
  8. Ada ya maombi ni Tsh. 100,000/= ambayo hazitarudishwa/ rejeshwa ilipwe kupitia akaunti
    22110030006 NMB (Jina Ufunuo Publishing House).
  9. Vitabu vya zabuni vinapatikana katika ofisi ya Ufunuo Morogoro Siku zote isipokuwa Jumamosi na Jumapili.
  10. Maombi yanatakiwa kufungwa kwenye bahasha iliyofungwa kwa lakiri na kuonyesha aina
    ya zabuni inayoombwa bila kuwa na viashiria vyovyote inakotoka na iwasilishwe katika
    ofisi ya Ufunuo Publishing House Morogoro, au itumwe kwa email [email protected]

N.B: Ramani/mchoro na nukuuza gharama ya ujenzi zinapatikana ofisi ya Ufunuo Morogoro,
muda na mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 14/06/2024 saa 4:00 asubuhi na Bodi itakapo kaa itawasiliana na waomba zabuni waliochaguliwa mchakato utakapo kamilika.

Ukiwa na wali wasiliana nasi [email protected]

MENEJA
UFUNUO PUBLISHING HOUSE

WhatsApp
Twitter
Email
LinkedIn
Instagram